lørdag 22. desember 2018

Greetings 08 - Danson Mwanyika


Kwa Ndugu zangu katika Kristo Yesu,

Nawasalimia kwa upendo wa Kristo Yesu. Bwana Yesu asifiwe wandugu na wadada.
Mimi Danson Mwanyika niko nyumbani hapa Taita. Mimi ni mzima na bado nampenda Kristo Yesu ambaye ni mwokozi wa maisha yangu na nafurahiya kuwa katika Kristo.
     Bado nawakumbuka kwa upendo wenu na hasa kwa kuipenda na kuitamani injili ya Kristo Yesu. Basi ningelipenda tushirikiane neno hili lipatikanalo kutoka kwa WAKOLOSAI 3:12 - 17.
      namshukuru sana ndugu Erling Lundeby ( namuita Mandevu ) kwa vile naona akiwa huko Ulaya anatukumbuka na hata akiwa hapo Kapenguria Mungu ambariki katika kazi hii yakueneza Injili yake Kristo.
      Wapendwa Mungu awabariki , moyo wangu nikiwa hapa Taita nimekuwa nikiwaza ni kwa njia gani nitaweza kuwasiliana ? Tumeachana katika mwili ila  tuko pamoja katika Roho. Kwa sasa nitapenda kupata adress za makanisa ya huko Chesta, Chepareria,Kapenguria na huko Sekker ili tuwe tukiwasiliana,  mujue vile ninaendelea na pia nijue vile mnaendelea. Nawashukuru sana kwa msaada wenu mlivyonisaidia na WImbi wakati nilipokuwa na ugonjwa wa Kisukari sasa sina shida hiyo ilipona kabisa na namshukuru Mungu. Lakini sasa. Mke wangu ndio shida inayomsumbua, tuendelee kumuweka kwa maombi.
     Mwisho nawatakia Krisimasi njema yenye baraka tukikumbuka kuwa Kristo Yesu alizaliwa ulimwenguni ili atuokoe kutoka kwenye dhambi.
ZABURI 27: 4 - 5
MUNGU AWABARIKI SANA. AMEN

MZEE DANSON MSAMI MWANYIKA






Ingen kommentarer: