lørdag 22. desember 2018

Greetings 01 - Astri Mangelrød Andersson


Wapendwa wa Pokot, 

Salamu nyingi kutoka mimi, "daktari" Astri. 
Mungu awabariki sana! 
Ninapokumbuka ninyi ninamshukuru Mungu sana! Asanta kwa kunipokea samani wakati wa Sekerr 1983-86 na 1987-88, Chesta 1987- 91! 
Wagonjwa walikuja, tulitembea mlimani upande wa Endow, Solion, Anett, Chemulokotyo na huko na huko. Isak Kataboyo alibeba mzigo yangu mara nyingi, Rosalyn alinisaidia nyumbani, Clementina na Eunice kwa clinic. Sisi sote tulihubiri na tulifundisha sundayschool. Wakati mwingine tulitembea usiku kwa wagonjwa, na niliendesha gari bila kufahamu tutaweza namna gani. Ninyi mlinisaidia, na Mungu alitulinda. Ninakumbuka furaha kubwa wakati watu walianza kuingia kanisa; wamama na wazee!!! Karam nyoman! 
Sasa mimi nimeanza kuwa mama mzee, lakini bado ninafanya kazi ya mwunguzi kati watu wenye cancer. Na bado ninampenda Yesu. Tungefanya  nini bila yeye? Ametusamehe, na ametulinda, na siku moja atatufungulia mlangu wa mbinguni. Huko tutakuwa pamoja! Praise HIM !! 

Maombi yangu kwa ninyi marafiki: Endelea kazi ile nzuri ambaye Mungu ameanza! Ninyi ni watu wake. 
Yesu anawapenda! 

Salamu kubwa kutoka hapo Norway! 

Dada Astri 
Kazi Miskwony.

Kazi Miskwony.

Mama yake Thomas Lokori

Thomas Riripon na Rosalyn wanasaidiana.

Mama wa Chemloktyo amezaa mtoto.

Miguu ya mzee.

Paulina, Sekerr.

Clementina na Astri wafanya pamoja.

Wamama wa Chesta.

Kijana wa Sekerr, nimesahau jina.

Ingen kommentarer: