lørdag 22. desember 2018

Greetings 03 - Bjørg and Asbjørn Vegge


Tuwasalamia ninyi, watu wote wa NWD/ELCK, ninyi mmefanywa watakatifu katika kuungana na Kristo Yesu, mkaitwa muwe wa Mungu, pamoja na watu wote popote wanaomwomba Bwana wetu Yesu Kristo aliye Bwana wao na wetu pia. 
Tuwatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba wetu na Bwana Yesu Kristo.
Twataka siku hii kubwa sana  ninyi nyote kuyapatia maneno Yesu Kristo, Mchungaji Mwema,  aliyeyasema: ” Kondoo wangu huisikia sauti yangu”. 
 ”Mimi nayatoa maisha yangu kwa ajili ya kondoo wangu.  Mimi nawajua, nao hunifuata.  Mimi nawapa uzima wa milele; nao hawatapotea milele, wala hakuna mtu atakayeweza kuwatoa mkononi mwangu.
 Neema yangu inatosha kwa ajili yao. 
Kaeni ndani yangu, nami nikae ndani yenu. Kaeni katika pendo langu.    Nimewaambieni mambo haya ili furaha yangu ikae ndaani yenu, na furaha yenu ikamilike.”
Salamu kutoka  Bjorg and Asbjorn  Vegge












Ingen kommentarer: